Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi

Historia

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa nyumba bora. Kwa miongo mingi Serikali zote kabla na baada ya uhuru zilitambua matatizo ya nyumba, umuhimu na uharaka wa kuyatatua.


Juhudi mbalimbali zimefanywa kushughulikia tatizo hilo. Ilifikiriwa kwamba ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili ni kuunda taasisi zitakazokuwa na wajibu wa kutoa mafunzo katika sekta ya nyumba ili kuboresha na kuongeza msingi wa ubora wa nyumba kutokana na tatizo kuendelea kuwapo. Serikali iliamua kuunda upya kituo cha Utafiti wa Ujenzi (BRU), kuwa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA), yenye mamlaka ya kuendesha shughuli kibiashara.

Office Location

Copyright © 2024 Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi Haki zote zimehifadhiwa. kanusho    MAKALA