Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi
Kama moja ya kazi ya matundu ni kupitisha mabomba ya umeme na kuimarisha kwa kumwaga rojorojo ya saruji katika kuta za kona ya jengo, kwenye madirisha na kwenye milango, Je wakati wa kumwaga zege ya lenta zege inayomiminwa si itaishia kwenye matundu?
Nondo zinazowekwa kwenye lenta zinazuia umwagikaji wa zege inayomiminwa.
Kwanini isitengenezwe mashine inayotumia umeme ama Hydraulic?
Gharama itakua kubwa sana na hivyo itaondoa unafuu wa utengenezaji tofali
Je kuna haja ya kupiga lipu kwenye nyumba iliyojengwa kwa kutumia matofali ya kufungamana?
Haina lazima hasa nje. Kwa ndani ni muhimu ili kupata finishing nzuri
Je nyumba hizi zinadumu miaka mingapi?
Zaidi ya miaka 45
Uimara wa nyumba zilizojengwa kwa kutumia teknolojia ya NHBRA ni upi.
Sawa na uimara wa tofali za block
Kwanini mashine ya vigae isitumie umeme badala ya betri ya gari.
Hii huiwezesha mashine kutumika sehemu yoyote hata isiyo na umeme (vijijini) ambako ndio kuna walengwa wakubwa.
Kwanini mashine ya matofali isitumie umeme ili kuwezesha kufyatua tofali nyingi kwa muda mchache.
Inawezekana lakini Wakala unawalenga watu wa kipato cha kati na chini ili waweze kujenga nyumba bora za gharama nafuu. Mashine ya umeme itakua na gharama kubwa.
Kwanini vigae vinalowekwa maji?
Kufanya viwe imara
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi
Po Box 1964
Mwenge, Dar es Salaam
Nukushi : +255222774003
Simu: +255222771971
Barua pepe: dg@nhbra.go.tz, dawatilamsaada@nhbra.go.tz Siku za kazi Jumatatu - Ijumaa Masaa ya kazi 01:30-09:30