Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu

 • Kwa kutambua kuwa nyumba ni moja ya mahitaji ya msingi kwa kila mtu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 ilianzisha Kituo cha Utafiti wa Vifaa vya Ujenzi, Nyumba na Majengo (BRU). Tarehe 31 Agosti 2001 kituo hiki kilibadilishwa kuwa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (National Housing and Building Research Agency – NHBRA). Madhumuni makuu yakiwa ni kufanya utafiti wa teknolojia na vifaa vya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu na kuzieneza kwa wananchi.

  Utafiti unaofanywa katika Wakala una lengo kuu la kuhakikisha kunakuwepo teknolojia rahisi za ujenzi wa nyumba na za gharama nafuu ili kuwezesha kila mtanzania kumudu gharama za kuboresha makazi yake. Hivyo ni matarajio yetu kwamba watanzania wenzetu watatambua uwepo wa teknolojia rahisi za ujenzi wa nyumba bora na kuzitumia katika kuboresha hali ya nyumba hapa nchini.

  Wakala upo wazi kushirikiana na mtu binafsi, taasisi za umma, na taasisi zisizo za umma katika kutekeleza lengo hilo. Hivyo basi, ninatoa wito kwa watanzania wote walio na wazo, au tayari wanayo teknolojia inayoweza kuboresha nyumba na makazi ya mtanzania kwa gharama nafuu, aje ashirikiane nasi katika kuifanyia tafiti teknolojia hiyo na kuisambaza kwa watanzania walio wengi ili faida yake iwafikie watanzania wengi iwezekanavyo.

  Kwa sasa Wakala unazo teknolojia za matofali ya kufungamana, vigae vya kuezekea, mashine za kutengenezea matofali, na mashine za kutengenezea vigae vya kuezekea. Watanzania wote wanakaribishwa kutembelea NHBRA au kuwasiliana nasi kwa anwani zilizopo katika tovuti hii ili kupata taarifa, ufafanuzi, au mafunzo ya kuweza kujitengenezea matofali na vigae vya kuezekea na pia kujenga kwa kutumia vifaa hivyo.

  Vilevile Wakala unatoa ushauri katika maeneo ya gharama za ujenzi, mbinu za ujenzi zinazoweza kupunguza gharama, usanifu wa nyumba bora za gharama nafuu na teknolojia nyingine za ujenzi wa gharama nafuu. Karibu sana, na ahsante kwa kutembelea tovuti hii. Tunatarajia kukuhudumia hivi karibuni.
  nyingine za ujenzi wa gharama nafuu. Karibu sana, na ahsante kwa kutembelea tovuti hii. Tunatarajia kukuhudumia hivi karibuni.

 • Office Location

  Copyright © 2017 Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi Haki zote zimehifadhiwa. kanusho    MAKALA